Peeling Off The Mask..

When the prime minister's adviser decides to sit us down and tell a story...


Former advisor to Prime Minister Raila Odinga, Miguna Miguna has finally launched his provocative memoirs in which he sharply criticizes Prime Minister Raila Odinga for allegedly condoning corruption. Miguna who wrote the book months after a bitter disagreement with Raila says the PM is not capable of fighting graft even if he became President.

The ICC have apparently taken Miguna's book as evidence and are to question him on holding Odinga responsible for 2007 unpeaceful stateThe full sotry is in Swa..
Miguna Miguna, aliyekuwa msaidizi wa Karibu wa zamani wa Waziri Mkuu wa Kenya na Mgombea Urais anayepewa nafasi kubwa kushinda kwenye uchaguzi mkuu ujao nchini humo, Bwana Raila ameikimbia Kenya.
Miguna alikuwa mshauri maalum wa kisiasa wa Bwana Odinga juu ya Mambo ya Serikali ya Mseto na alifukuzwa kwenye nafasi hiyo agosti 4 mwaka jana kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.
Juzi Jumamosi Bwana Miguna alizindua kitabu kilichopata umaarufu wa hali ya juu kiitwacho "PEELING BACK THE MASK" ambacho kimeelezea kwa kirefu juu ya aliyoyaita Mapungufu, "Udhaifu", Mabaya, Siasa chafu na Mambo ya siri ya Bwana Raila Odinga.
Miguna amekwenda mbali zaidi kwa kumhusisha Raila na chama chake cha ODM juu ya machafuko yaliyosababishwa na ghasia za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007, jambo amabalo limezua majadala mkubwa na malumbano ya kutaka bwana Migunaa ahojiwe na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC kwa tuhuma hizo alizozitoa.
Mkurugenzi wa Mashtaka Mkuu wa Kenya, DPP Keriako Tobiko pamoja na Mkuu wa Polisi wa Kenya, Bwana Mathew Iteere nao waliingia kwenye malumbano yaliyozushwa na kauli hiyo ya Miguna kwa kumtaka Miguna akahojiwe na ICC na yeye kwa ujeuri amewaita "wachekeshaji wasiojua wafanyalo", kwa kuwa wao (Tobiko na Iteere) si wafanyakazi wa Mahakama ya ICC na hawana uhakika kama amehojiwa au hajahojiwa na Mahakama ya ICC.
Hayo yote yamewaudhi wafuasi wa Raila na ODM na hivyo kuchochea tishio la usalama wa Miguna na Familia yake, jambo amabalo ndilo limeonekana kupelekea Miguna kuikimbia Kenya.
Usiku wa Jumatatu Miguna, Mkewe pamoja na watoto wao watatu walionekana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi wakiondoka na Ndege kuelekea Canada.
Askari Polisi aliyewashuhudia Uwanjani hapo alisema kuwa bwana Miguno alionekana kuwa na mizigo mingi wakati akiondoka
Raila's reply here