Ray C Pays The President a Visit

She is my Favorite Tanzanian female artist and it was heartbreaking when we all discovered what state she was in after drug abuse.
She recently went to the White house to Thank Mister President Jakaya Kikwete for helping her through treatment.


Brought tears to my eyes how Generous our president is to lift a finger and help out this young artist who was lost and in need as everyone else was quick to judge, blame and point fingers. Viva The President. Man of the people.

Msanii wa Kizazi Kipya hapa nchini ,maarufu kama Bongo Flavour, Bi Rehema Chalamila anaejulikana zaidi kama Ray C, leo mchana amefika Ikulu ya Dar-Es-Salaam kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa msaada mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika jijini Dar-Es-Salaam chini ya uangalizi maalum
Ray C amefika Ikulu akiongozana na mama yake mzazi Bibi Margareth Mtweve ambaye pia amemshukuru Rais Kikwete kwa msaada huo mkubwa ambao umesaidia kurudisha hali ya kawaida ya Ray C.
Rais amempongeza Ray C kwa kukubali hali yake ya kiafya na hatimaye kukubali kupata matibabu ambayo bado anaendelea nayo chini ya uangalizi maalum.
Rais amemtaka mwanamuziki huyo kufuata masharti ya madaktari ili aweze kupona kabisa na hatimaye kurudia hali yake ya mwanzo na kurejea katika shughuli zake za kujitafutia kipato na maisha.
Kwa vile Ray C bado yuko katika matibabu, hatutaweka wazi sehemu anayotibiwa hadi atakapokuwa tayari kabisa kurudi katika shughuli zake rasmi hivyo tunaomba jamii impe ushirikiano huo na kuheshimu taratibu zake za matibabu ili hatimaye aweze kupona kikamilifu.
“MWISHO”Imetolewa na :Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-DSM10 Desemba, 2012