Kilimanjaro Music Awards Social Media Lounge


Kilele cha tuzo za Muziki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Music Awards kinatarajia kufanyika siku ya Jumamosi, Juni 8 katika ukumbi wa Mlimani City kwa kuwapa tuzo wasanii waliofanya vizuri katika  kipindi cha mwaka 2012. Kwa mara ya kwanza mwaka huu kutakuwa na tukio la Red Carpet ambapo watu maarufu watapita kupiga picha na kufanya mahojiano ya moja kwa moja na muendeshaji ambaye ni mtangazaji wa kituo cha Channel O, Jokate Mwegelo. Tuzo hizi zitaonyeshwa live kupitia katika mtandao wa Internet huku watumiaji wa simu za mikononi na kompyuta wasioweza kufuatilia kupitia TV zao wakiweza kutazama mtandaoni katika ukurasa wa Facebook wa Kilimanjaro Premium Lager (www.facebook.com/kilimanjaropremiumlager) na pia mtandao wa LIVESTREAM (http://new.livestream.com/KTMA2013/live) .  Wakati wa zoezi la utoaji tuzo washindi wote watapata nafasi ya kuongea na  kuwashukuru mashabiki katika Social Media Lounge itakayoendeshwa na Millard Ayo kutoka Clouds FM na Sam Misago kutoka East Africa TV. Picha za matukio na kinachoendelea katika ukumbi wa Mlimani City zitakuwa zikirushwa moja kwa moja katika mtandao wa Twitter na Instagram ambayo ni ( @Kili_Lager).