The Presidents Speech

It sure took Mr. President a long time to respond to the ill comments from Rwandan leaders/Politicians along with their president Paul Kagame who 2 months ago stated“Those people [Tanzanian President Jakaya Kikwete] you just heard siding with Interahamwe and FDLR  and urging negotiations… negotiations?  Me, I do not even discuss this topic, because I will just wait for you [Tanzanian President Jakaya Kikwete] at the right place and I will hit you! He[Tanzanian President Jakaya Kikwete]  did not deserve my answer. I did not waste my time answering him…It is well known. There is a line you cannot cross, there is a line, a line that you should never cross. It is impossible…” While adressing Rwandan Youth on June 30, 2013 during a summit called “Youth Konnect”


Well, His Honorable Mr. President Jakaya M Kikwete Finally Responded, in a monthly speech aired on National Television TBC on July 31st 2013
'For Godsakes Paul you drama queen Shut Up already,' he said  ' If  you dont want my advice just shut up, I told Museveni the same thing and he's not crying around'  He continued 'Either way I dont have time for this  and dont threaten me, remember Idd Amin? Oh and If you're going to insult me say it to my face '  He finished. 

Well , he didnt actually use those exact words  sigh and my summation of events might come off  a little dramatic but hey...A close enough translation to his excellency's kind diplomatic wise words . The whole fiasco is just really uncalled for, I think President Paul Kagame  shouldn't have verbally attacked our president like that so undiplomatic and our president so coolly handled the situation,No uncalled for drama. Listen to the speech and read his full response on Rwanda below.  


          Elaborating his Kagera Speech which Sparked Controversy
 Katika hotuba yangu pale Kaboya niliwakumbusha Watanzania wenzangu kwamba katika kuwakumbuka mashujaa wetu wale na sisi tulio hai, hatuna budi kutambua wajibu wetu wa kuwa tayari kujitolea muhanga kwa ajili ya kulinda uhuru wa mipaka ya nchi yetu.  Nilisisitiza utayari wa nchi yetu kulinda mipaka yake na kwamba mfano wa mashujaa waliolala pale ni fundisho kwa mtu ye yote anayetamani kumega kipande cho chote cha ardhi ya nchi yetu.  Atakiona cha mtema kuni kilichomkuta Nduli Iddi Amini  au hata zaidi.
Nimesikia kuwa kauli yangu ile imetafsiriwa visivyo na kupotoshwa na baadhi vyombo vya habari na hata majirani zetu.  Tafsiri hizo ni potofu. Sikumtaja mtu ye yote au nchi yo yote.  Nilikuwa nazungumzia wajibu wa majeshi yetu na raia wa nchi yetu wa kulinda uhuru na mipaka yetu na kwamba hatutamruhusu mtu au nchi yo yote kutupokonya wala kuichezea haki yetu hiyo ya msingi.  Tuko tayari kuitetea hata kama gharama yake ni maisha yetu kama walivyofanya mashujaa waliolala Kaboya. 

Response to Rwanda 
Ndugu wananchi;
Katika kipindi cha miezi miwili sasa hususan tangu mwishoni mwa mwezi Mei, 2013, uhusiano baina ya nchi yetu na Rwanda unapitia katika wakati mgumu.  Kauli za viongozi wa Rwanda dhidi yangu na nchi yetu ni ushahidi wa kuwepo hali hiyo.  Napenda kuwahakikishia Watanzania wenzangu na ndugu zetu wa Rwanda kuwa mimi, Serikali ninayoiongoza na wananchi wa Tanzania tunapenda kuwa na uhusiano mzuri na ushirikiano wa karibu na Rwanda kama ilivyo kwa nchi zote jirani.  Kama majirani kila mmoja anamuhitaji mwenzake, hivyo lazima tuwe na uhusiano mwema na ushirikiano mzuri.

Napenda kusisitiza kuwa mimi na Serikali ninayoiongoza tutakuwa wa mwisho kufanya kitendo au vitendo vibaya dhidi ya Rwanda au nchi yo yote jirani au yo yote duniani.  Hatuna sababu ya kufanya hivyo kwani ni mambo ambayo hayana tija wala maslahi kwetu.
Ndugu Wananchi;
Ukweli ni kwamba wakati wote tumekuwa tunajihusisha na mambo ya kukuza na kujenga ujirani mwema na kufanya mambo ambayo yatasaidia kuimarisha uhusiano wetu kwa maslahi ya nchi zetu.  Hiyo ni moja ya nguzo kuu ya Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania. Huo ndiyo ukweli kuhusu uhusiano wetu na nchi ya Rwanda kabla na hata baada ya sintofahamu iliyojitokeza sasa. 
  Napenda kuwahakikishia ndugu zetu wa Rwanda kuwa kwa upande wetu hakuna kilichobadilika wala kupungua katika uhusiano na ushirikiano wetu. Mambo yapo vile vile. Kwa upande wangu, binafsi, sijasema lo lote kuhusu Rwanda pamoja na maneno mengi ya matusi na kejeli yanayotoka kwenye vinywa vya viongozi wa Rwanda dhidi yangu.  Siyo kwamba siambiwi yanayosemwa au sijui kusema au sina la kusema, la hasha. Sijafanya hivyo kwa sababu sioni faida yake.  Kwangu mimi sioni kama kuna mgogoro wa aina yo yote.   Busara inatuelekeza kuwa tusikuze mgogoro usiokuwepo.  Waingereza wanasema “two wrongs do not make a right”.
Ndugu Wananchi;
Kama mjuavyo uhusiano wetu na Rwanda umekuwa mzuri kwa miaka mingi.  Tunashirikiana na kusaidiana kwa mambo mengi baina ya nchi zetu kitaifa na katika kanda yetu ya Afrika Mashariki na Nchi za Maziwa Makuu, katika Umoja wa Afrika na hata kimataifa.  Uhusiano unaelekea kupata mtikisiko baada ya mimi kutoa ushauri kwa Serikali ya Rwanda kuzungumza na mahasimu wao.  Ushauri ule niliutoa kwa nia njema kabisa kwani bado naamini kuwa kama jambo linaweza kumalizwa kwa njia ya mazungumzo njia hiyo ni vyema itumike.  Isitoshe, ushauri ule niliutoa pia kwa Serikali ya Kongo na kwa Serikali ya Uganda.  Katika mkutano ule Rais Yoweri Museveni wa Uganda aliunga mkono kauli yangu. Rais wa Rwanda hakusema cho chote pale mkutanoni.  Baada ya kurudi nyumbani ndipo tukaanza kuyasikia maneno tuliyoyasikia na tunayoendelea kuyasikia.
Kwa kweli nimestaajabu sana na jinsi walivyouchukulia ushauri wangu na wanayoyafanya.  Havifanani kabisa, completely out of proportion and out of context. Mimi nilifanya vile kwa kuzingatia mila na desturi zetu za miaka mingi katika ukanda wetu.  
 Tumekuwa tunakutana katika mikutano na vikao mbalimbali tunazungumza na kushauriana kwa uwazi juu ya njia za kushughulikia matatizo na masuala mbalimbali kila yanapotokea.  Wakati wote tumeyachukulia kuwa ni mambo yanayotuhusu sote hivyo kupeana ushauri ni wajibu wetu wote.  Na mara nyingi ushauri kwa wanaogombana kuzungumza tunautumia sana.  Iweje leo mtu kutoa ushauri ule lionekane jambo baya na la ajabu.  Jambo la kushutumiwa na kutukanwa!  Siyo sawa hata kidogo!! Ushauri si shuruti, ushauri si amri.  Una hiyari ya kuukubali au kuukataa. 
 Muungwana hujibu:  “Siuafiki ushauri wako”.  Hakuna haja ya kutukana wala kusema maneno yasiyostahili wala kusema yasiyokuwepo na ya uongo.
Ndugu Wananchi;
Napenda kurudia kusema kuwa mimi binafsi na Serikali yetu ya Tanzania hatuna ugomvi wala nia yo yote mbaya na Rwanda.  Tunapenda tuendelee kuwa na uhusiano mzuri na Rwanda.  Labda wenzetu wanalo lao jambo dhidi yetu ambalo sisi hatulijui.  Maana na sisi tunasikia mengi yanayozungumzwa na kudaiwa kupangwa kufanywa na Rwanda dhidi yangu na nchi yetu.  Hatupendi kuyaamini moja kwa moja tunayoyasikia lakini hatuyapuuzi.