Joke of the Day

From Anko Kitime, laughed myself silly
Tamko kutoka Chama cha Maboifrend Tanzania (CHAMATA)
 Wapenzi wetu, wake zetu, nyumba ndogo zetu, samsing zetu, dogodogo zetu, kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu kama vile;
·      uchaguzi wa Madiwani katika kata 27
·      moto uliotokea mara kadhaa katika masoko ya Mbeya
·      majukumu ya mambo ya shule mwezi January
·      vipigo visivyoisha vya Manchester United
·      ukijumlisha na kipigo kibaya cha Arsenal dhidi ya Liverpool wiki iliyopita
·      kuhamishwa wa viongozi wa polisi karibuni
·      mtafaruku wa Zitto Kabwe na CHADEMA
·      vita vya Sudan Kusini
·      kuongezeka kwa rushwa
·      ujangili wa meno ya tembo
·      kukamatwa kwa shehena kubwa ya madawa ya kulevya
·      uteuzi wa Bunge la Katiba
·      kuongezeka kwa gharama za umeme
·      msongamano wa magari barabarani na mengine mengi sana
Tungependa kutoa taarifa mapema kwamba hatutashiriki wala kuwepo katika sherehe za Valentine mwaka huu.
Nchi yetu inahitaji kufunga na maombi wakati huu, na sisi, kama sehemu ya Taifa letu tumeamua kuwa katika mfungo wa kuombea nchi yetu kuanzia tarehe 12 hadi 16 February mwaka huu. Tunashauri na nyinyi mchukue muda huo mwafaka, kusherehekea Valentine na wazazi wenu kwani nao ni sehemu ya mapenzi ya Valentine.
Tunategemea kukutana nanyi tena tarehe 17 na tunashukuru kwa ushirikiano ambao tuna uhakika mtauonyesha katika kipindi hiki kigumu cha kuliombea taifa letu Tanzania

MWENYEKITI TAIFA
CHAMATA


Chama cha Magelofrend Tanzania (CHAMGATA) kimetoa tamko lifuatalo......
SISI MAGELOFREND TANZANIA, VALENTINE HII HATUTAKI MAUA, WALA, IPHONE, WALA IPAD, WALA PESA, WALA DINA, WALA LANCHI. TUNASISITIZA MABOYFRIEND WETU SIKU YA TAREHE 14 FEBRUARI WAJE WAJITAMBULISHE KWA WAZAZI WETU NA KUTOA TAREHE YA HARUSI...KAULI MBIU MWAKA HUU NI...HARUSI KWANZA.....
Mwenyekiti
CHAMGATA